Kuwekeza Furniture huu ni Mpango wa Kubandika umeundwa kwa ajili ya kusaidia wateja wetu kulipia bidhaa kwa awamu bila mzigo mkubwa wa kifedha. Kalkuleta hii hukupa makadirio ya kianzio, malipo ya kila mwezi, na gharama ya mwisho ikiwa utachelewa. Tunahimiza ulipaji wa haraka ndani ya miezi mitatu ili kuepuka ongezeko la 10%. Tumia kalkuleta hii kupanga bajeti yako vizuri kabla ya kuanza mchakato wa malipo. Karibuni Sana
🛠️ Kalkuleta ya Malipo
🪑 Mpango wa Kubandika/Kuwekeza Furniture
Table of Contents
Sheria na Ratiba za Ubandikaji wa Samani – Utaipenda Furniture
Kama ilivyoelezwa kwenye ukurasa wa Namna na Mfumo wa Ulipaji, Utaipenda Furniture imejenga mfumo rahisi wa upatikanaji wa samani za majumbani na maofisini kupitia mpango wetu wa Kubandika au Kuwekeza Furniture. Lengo letu ni kuwafikia watumiaji wote wa fenicha kwa njia ya kiurahisi, kiuwazi, na yenye heshima kwa uwezo wa kifedha wa kila mteja.
📘 Maana ya Kubandika/Kuwekeza Furniture
Hii ni njia ya kulipia bidhaa au huduma kidogo kidogo hadi mteja atakapokamilisha malipo yote ndipo bidhaa yake itakapotolewa au huduma kutekelezwa. Ni suluhisho bora kwa mtu mwenye bajeti ndogo lakini anayehitaji bidhaa bora.
⚖️ Kanuni na Masharti ya Mpango
1. 💰 Kianzio cha Awali
- Mteja anatakiwa kutoa kianzio cha angalau 20% ya bei ya bidhaa.
- Kwa kila Tsh 100,000, unatanguliza Tsh 20,000.
Mfano:
Kabati la milango mitatu
Bei: Tsh 380,000
Kianzio = 380,000 × 20% = Tsh 76,000
2. ⏳ Muda wa Malipo na Ongezeko la 10%
- Malipo yanapaswa kukamilika ndani ya miezi mitatu.
- Ukichelewa, ongezeko la 10% litaongezwa kwenye kiasi kilichobaki kwa kila kipindi cha miezi mitatu kinachofuata.
Mfano:
Umeanza na kianzio Tsh 80,000
Baada ya miezi mitatu umelipa Tsh 300,000
Deni lililobaki = Tsh 80,000
Ongezeko = 80,000 × 10% = Tsh 8,000
Jumla ya deni = Tsh 88,000
Lengo letu ni kuhakikisha bidhaa inakamilika ndani ya miezi mitatu. Kukaa na deni kwa muda mrefu huongeza gharama za usimamizi wa kumbukumbu.
3. 🧾 Risiti na Gharama Zake
- Jumla ya risiti zinazotolewa bila malipo ni moja tu.
- Risiti zote zinazofuata zitatozwa Tsh 500 kila moja.
Mfano wa Kabati la Milango Mitatu:
- Kianzio: Tsh 80,000 → Risiti ya Kwanza (Bure)
- Mwezi wa Kwanza: Tsh 100,000 → Risiti ya Pili (Tsh 500)
- Mwezi wa Pili: Tsh 100,000 → Risiti ya Tatu (Tsh 500)
- Mwezi wa Tatu: Tsh 100,000 → Risiti ya Nne (Tsh 500)
Jumla ya gharama za risiti = Tsh 1,500
4. 🛠️ Kuanza kwa Utengenezaji au Huduma
- Bidhaa huanza kutengenezwa baada ya malipo ya angalau 70% ya bei.
- Huduma huanza kutekelezwa baada ya malipo ya 80%, na uthibitisho wa uwezo wa kumalizia.
Mfano:
Kabati la Tsh 380,000
70% = Tsh 266,000
Kwa mpangilio wa kawaida, kazi huanza baada ya malipo ya tatu.
5. 📦 Upokeaji wa Bidhaa
- Bidhaa hukabidhiwa ndani ya siku 7 za kazi baada ya kumaliza malipo.
- Sikukuu za kitaifa hazihesabiwi kama siku za kazi.
Mfano:
Umemaliza malipo tarehe 5/8
Sikukuu ni tarehe 8/8
Siku 7 za kazi = kati ya tarehe 6/8 hadi 13/8
🟢 Tunathamini Uelewa Wako
Mpango huu umeundwa kwa uwazi, heshima, na lengo la kukuwezesha kupata samani bora bila mzigo wa kifedha. Tunakukaribisha kujiunga na mpango wa Kubandika/Kuwekeza na kufurahia huduma ya kipekee kutoka Utaipenda Furniture. Ili Kurahisha Mahesabu tumeweka Kalkuleta Hapo juu
Kwa Maelezo zaidi Wasiliana nasi Kupitia Namba : 255 683 8067 52